by Shabaan Otieno, Mziwanda Banda
- ISBN: 9789966562845
- SKU: 2010127000709
Kiswahili Angaza ni kazi iliyosukwa na kuwambwa kwa makini na kwa kina kirefu. Imetimiza kwa ukomo wa ukamilifu mahitaji ya mtalaa mpya wenye kuzingatia umilisi, yaani, Competency-Based Curriculum, 2018. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo unaomwegemea mwanafunzi zaidi na kumfanya mwalimu awe mwelekezi tu wala si mtoaji wa elimu. Kitabu hiki kinazingatia mambo matano muhimu: 1. Kusoma ni kutagusano; wanafunzi wanafanya Shughuli mbalimbali wakiwa peke yao, wawili wawili au katika makundi; 2. Wanafunzi wanaanza kila somo kwa kuelezea picha au hall ama matukio wanayoyafahamu huku wakijadiliana; 3. Wanafunzi wanashiriki katika stadi nyingi za kufikiria kama vile kuchanganua, kutambua, kubainisha, kujenga na kuhakiki; 4. Lugha iliyotumika ni nyepesi mno no isiyokuwa na maneno magumumagumu na misamiati ya kubabaisha; 5. Mwanafunzi na mwanafunzi mwenzake, pamoja na mwalimu, mzazi na hata jarnii nzima wanashirikishwa ndani ya kitoau hiki.